Kampuni ya Pantone Color Institute imeitangaza rangi hii ya zambarau isiyokoza sana kuwa rangi rasmi itakayotumika rasmi atika shughuli mbalimbali za mitindo , harusi, kwenye matamasha mbali mbali pamoja na mitoka tofauti tofauti
Pantone Color Institute ni kampuni kubwa duniani inayohusika na kujikita na utafiti wa rangi katika tasnia ya mitindo (fashion) na kutoa ushauri wa matumizi ya rangi, pia saikolojia kwa wavaaji pamoja na maana zake na ilihusika kufanya uteuzi wa rangi hizi za mwaka tangu mwaka 2000
Lakini pia Pantone hufanya kazi kwa makampuni ya mitindo na urembo duniani za ubunifu na uchanganyaji wa rangi ya mavazi
Rangi hii ya UTRA VIOLET PURPLE inamaanisha upekee wa kila mtu yenye kusimamia uhalisi, uelekevu na usawa kwa watu
Kwa mwaka 2018 mapambo malimbali yatahusika katika mchanganyiko wa rangi mbalimbali ikihusisha rangi ya Purple katika kumbi za sherehe za harusi, mwago(Sendoff), kitchen party bila kusahau kuta na sebule za nyumba za watu
Baadhi ya watu maarufu na mashuhuri wakiwemo wasanii, wanamitindo na wanasiasa wamepambaika na mavazi yaliyosheheni rangi hii au yaliyochanywa na rangi hii katika shughuli, mitoko na maonyesho kadhaa duniani
Toa maoni yako katika ukurasa wetu wa faceboook KIJUZI
AU kwenye E-Mail yetu, kijuziblog@gmail.com