ISRAEL YASHAMBULIA DAMASCUS HUKO SYRIA

 

Ripoti hizo zimetangazwa leo Jumatano na shirika la habari la SANA linaloendeshwa na serikali ya Syria.

Shirika hilo bila ya kutowa ufafanuzi zaidi limesema mashambulizi ya Israel yamelenga eneo la makaazi la Kafr Sousa huku wakaazi wa eneo hilo wakiliambia shirika la habari la kijerumani DPA kwamba walisikia sauti za miripuko na kuona moto ukiwaka kwenye baadhi ya nyumba za watu katika jengo moja lililoko karibu na shule.

Shirika linalofuatilia hali ya haki za binadamu nchini Syria lenye makao yake Uingereza limesema
hii ni mara ya 13 Israel kuishambulia Syria mwaka huu.