WAZIRI MKUU UINGEREZA AKUTANA NA MKENYA ALIYEDAIWA KUUAWA



Naibu Waziri wa Majeshi wa Uingereza James Heappey ameahidi kukutana na familia ya mwanamke Mkenya anayedaiwa kuuawa zaidi ya muongo mmoja uliopita na mwanajeshi wa Uingereza.

Bw Heappy alikuwa akizungumza katika ziara yake nchini, ambapo kisa hicho kimezua ghadhabu kubwa huku kukiwa na madai ya kufichaukweli kuhusu kilichotokea

Miaka 12 iliyopita walioshuhudia wanasema Agnes Wanjiru aliondoka kwenye baa moja na wanajeshi wawili wa Uingereza.

Miezi mitatu baadaye mwili wake ulipatikana kwenye shimo la maji taka karibu na kambi ya jeshi la Uingereza.

Naibu Waziri wa Ulinzi wa Uingereza anayesimamia jeshiJames Heappey aliambia BBC kwamba anaelewa uchungu wa familia ya Bi Wanjiru.

Alisema alifurahi kukutana nao na kujadiliana na kuelewana kadri awezavyo.

Mwaka jana mpwa wake aliandika barua ya wazi akiomba kukutana na Mfalme Charles wakati wa ziara yake nchini, akisema maafisa wa Uingereza hawakuonekana kujali.

Alisema atakaribisha kutembelewa na Bw Heappey baada ya zaidi ya muongo mmoja wa maumivu na kufadhaika.

Uchunguzi wa Kenya ulihitimisha kuwa askari mmoja au wawili wa Uingereza walikuwa walimuua Agnes Wanjiru, na polisi walifungua uchunguzi baada ya madai ya nja ya kuficha mauaji hayo. Lakini bado hakuna aliyeshtakiwa.

Bw Heappey alisema Uingereza itaunga mkono maombi yoyote ya kurejeshwa nchini humo

Chanzo; BBC SWAHILI