DAR ES SALAAM WATAKIWA KUHIFADHI MAJI

 


Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imetoa taarifa kwa Wateja wake na Wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Chini kuwa, kutakuwa na upungufu wa huduma ya maji kwa baadhi ya maeneo ili kuruhusu maboresho ya msingi katika mtambo leo Jumanne March 5,2024 kuanzia saa 12 jioni hadi Alhamisi March 7,2024.

Maeneo yatakayoathirika na upungufu huu wa huduma ya maji ni Bagamoyo, Mapinga, Mabwepande, Bunju, Tegeta, Kunduchi, Mbweni, Boko, Salasala, Goba, Mivumoni, Madale, Goba, Kawe, Lugalo, Makongo, Chuo Kikuu UDSM, Mwenge, Chuo Kikuu Ardhi, Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Oysterbay, Masaki, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Kigogo, Chang’ombe, Keko, Kurasini, Kigamboni, Airport, Kiwalani, Buguruni, Vingunguti, Ilala na Katikati ya Jiji.

“DAWASA inawashauri Wananchi kuhifadhi maji ya kutosha katika kipindi cha matengenezo” ——— imeeleza taarifa ya DAWASA.